Timu ya taifa ya Rwanda chini ya umri wa miaka 20 watakutana uso kwa uso na timu ya taifa ya Moroko chini ya miaka 20 ikiwa ni mechi ya kumbukumbu ya mauwaji ya kimbari itakayochezwa Juni 18 katika uwanja wa Amahoro mjini Kigali.
Mchezo huo utakaochezwa itakuwa ni sehemu ya maadhimisho kwa zaidi ya watusi milioni moja waliopoteza maisha yao mwaka 1994.
Mwaka jana uzinduzi wa michuano hiyo ya kuadhimisha mauwaji ya kimbari iliwavutia timu nne kuu za Kenya ,Sudani Kusini, Tanzania na mwenyeji wao Rwanda.
No comments:
Post a Comment