Pages

Wednesday, 15 June 2016

RWANDA KUKUTANA NA MOROKO KUMBUKUMBU YA MAUWAJI YA KIMBARI

Timu ya taifa ya Rwanda chini ya umri wa miaka 20 watakutana uso kwa uso na timu ya taifa ya Moroko chini ya miaka 20 ikiwa ni mechi ya kumbukumbu ya mauwaji ya kimbari itakayochezwa Juni 18 katika uwanja wa Amahoro mjini Kigali.
Mchezo huo utakaochezwa itakuwa ni sehemu ya maadhimisho kwa zaidi ya watusi milioni moja waliopoteza maisha yao mwaka 1994.
Mwaka jana uzinduzi wa michuano hiyo ya kuadhimisha mauwaji ya kimbari iliwavutia timu nne kuu za Kenya ,Sudani Kusini, Tanzania na mwenyeji wao Rwanda.

Mauaji ya Kimbari ya Rwanda yalikuwa mauaji ya halaiki nchini Rwanda mnamo mwaka wa 1994 ambapo Watutsi, Watwa na baadhi ya watu wa kabila la Kihutu waliuliwa na serikali iliyosimamiwa na viongozi wa Kihutu.

No comments:

Post a Comment