Klabu ya mpira wa miguu Barcelona imekubali kulipa faini ya Euro milioni 5.5 kwa makosa ya uhamisho wa mchezaji wa kimataifa wa Brazil Neymar mwaka 2013.
Rais
wa Klabu hiyo Joseph Maria Bartomeu
amesema kuwa kulikuwa na tatizo katika ulipaji wa kodi katika uhamishio wa
Neymar.
“tumekubali
kulipa faini ya Euro milioni 5.5 kwa kosa lililofanyika mwaka 2011 na 2013 kama
mpango wa kodi wakati wa usajili wa Neymar” alisema Rais Bartomeu
Barcelona
imekuwa ikituhumiwa kwa udanganyifu wa kodi wakati wa usajili wa Neymar jambo
ambalo uongozi wa Barcelona umekuwa ukikataa kwa muda mrefu.
Neymar
na baba yake pia wanachunguzwa kwa kile kinachoitwa kuwa ni ukwepaji wa kodi
jamba ambalo pia na wao wanakataa.
Neymar
Da Silva Santos Junior alijiunga na Barcelona
June 2013 baada ya mafanikio aliyoyapata akiwa na clabu yake ya Santos
ya nchini Brazil.
| Neymar (kushoto) Rais Bartomeu |
No comments:
Post a Comment