Wednesday, 15 June 2016

SHARAPOVA: ITF HAIJANITENDEA HAKI

Mshindi mara tano wa Grand Slam Maria Sharapova anatafuta njia ya kutaka kupunguzwa au kufutiliwa mbali adhabu ya kufungiwa miaka miwili kwa kosa la kungundulika kutumia dawa zilizokatazwa michezoni.

Sharapova amekata rufaa ya adhabu hiyo katika mahaka ya usuluhishi ya michezo (CAS) jana jumanne.
Mchezaji huyo wa tennis wa Urusi mwenye miaka 29 alifungiwa na Chama Cha Tenis Cha kimataifa (ITF) mapema mwezi huu kufuatia vipimo vilivogundua kuwa anatumia dawa zilizokatazwa michezoni katika michuano ya wazi ya Australia.
maria sharapova, sharapova, maria sharapova ban, sharapova ban, tennis news, tennis
Maria Sharapova(AP)

No comments:

Post a Comment