Wednesday, 8 June 2016

Vardy akausha uhamisho wake kwenda Arsenal

Nyota wa Leicester City Jamie Vardy amesalia kimya kuhusu uwezekano wake wa kuhamia klabu ya Arsenal.
Mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 29 alipangiwa kuamua iwapo atasalia na Leicester au atajiunga na Gunners kabla yake kusafiri kuelekea Ufaranca kushiriki michuano ya Euro 2016 itakayong’oa nanga Ufaranza Jumatatu.
Lakini ameabiri ndege pamoja na wenzake wa timu ya taifa ya England bila kufahamisha Arsenal uamuzi wake.
Vardy bado anatarajiwa kufanya uamuzi kuhusu ofa ya Arsenal ya kumuahidi ujira wa £120,000 kila wiki baadaye leo Jumatatu.
Vardy

No comments:

Post a Comment