Wednesday, 15 June 2016

SANCHEZ AIPELEKA CHILE ROBO FAINALI

Magoli mawili ya Alexis Sanchez na mawili ya  Eduardo Vargas yameipeleka Chile hatua ya robo fainali katika michuano ya Copa America kwa ushindi wa goli 4-2 dhidi ya Panama mchezo uliopigwa jana Jumanne.
Chile ambaye pia ni bingwa mtetezi itakutana na Mexico katika hatua ya robo fainali itakayochezwa siku ya Jumamosi.
ukiachia matokeo hayo, Agentina pia iliilaza Bolivia kwa jumla ya magoli matatu kwa bila.

Alexis Sanchez na Eduardo Vargas(Super Sport)

No comments:

Post a Comment