Tuesday, 14 June 2016

BARCELONA: YA NEIMAR BORA YAISHE


Klabu ya mpira wa miguu Barcelona imekubali kulipa faini ya Euro milioni 5.5 kwa makosa ya uhamisho wa mchezaji wa kimataifa wa Brazil Neymar mwaka 2013.

Rais wa Klabu hiyo  Joseph Maria Bartomeu amesema kuwa kulikuwa na tatizo katika ulipaji wa kodi katika uhamishio wa Neymar.

“tumekubali kulipa faini ya Euro milioni 5.5 kwa kosa lililofanyika mwaka 2011 na 2013 kama mpango wa kodi wakati wa usajili wa Neymar” alisema Rais Bartomeu

Barcelona imekuwa ikituhumiwa kwa udanganyifu wa kodi wakati wa usajili wa Neymar jambo ambalo uongozi wa Barcelona umekuwa ukikataa kwa muda mrefu.

Neymar na baba yake pia wanachunguzwa kwa kile kinachoitwa kuwa ni ukwepaji wa kodi jamba ambalo pia na wao wanakataa.

Neymar Da Silva Santos Junior alijiunga na Barcelona  June 2013 baada ya mafanikio aliyoyapata akiwa na clabu yake ya Santos ya nchini Brazil.
Neymar da Silva Santos Junior and Barcelona president Josep Maria Bartomeu
Neymar (kushoto) Rais Bartomeu

No comments:

Post a Comment