Tuesday, 27 September 2016

TIMU ZA KAMPENI ZARIDHISHWA NA WAGOMBEA WAO



TIMU ZA KAMPENI ZA URAIS ZARIDHISWA NA MAJIBU YA WAGOMBEA


Timu za kampeni kwa Hillary Clinton na Donald Trump wote wameridhishwa na mwenendo ya wagombea wao katika mdahalo wao wa kwanza wa televisheni wa kampeni za urais Marekani. Wagombea hao mahasimu wa walikuwa wakikwazana mara kwa mara. Bwana Trump alimshtumu bi Clinton  kwa kuwa mwanachama wa uzalishaji mbovu wa kisiasa. Na Bi Clinton alisema mhasimu wake amekuwa ni aina ya mtu ambaye anawezakukasisishwa na twita na asingepaswa kunyoosha vidole vyake popote karibu na kodi za Nuclia za Marekani.
 


SHAMBULIO BAGHDAD LOAWAUWA WATU 11 NA KUJERUHI ZAID YA 50
Shambulio la bomu katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad,limewauwa watu kumi na mmoja na kuwajeruhi zaid ya watu hamsini. Kundi la I-S limedai kuhusika kwa mashambulio hayo,likisema mmoja ya wapiganaji wake alijilipua katika eneo linalokaliwa na waislimau wengi wa madhehebu ya shia mjini Baghdad wilaya ya Jadida,likiwauwa watu nane. Shambulio jengine lililenga la mauwaji lililenga eneo la Bayaa kusini mwa Baghdad,likiwauwa watu tisa.Mwaka huu umeshuhudiwa idadi kubwa ya mashambulizi ya I-S katika mji mkuu wa Iraq, wakati kundi hilo likipoteza baadhi ya majimbo maeneo mengine ya nchi hiyo.

 

No comments:

Post a Comment