Ripoti kutoka Alepo inasema vikosi vya
serikali ya Syria vimeendelea kuimarika katikati mji huo. Waasi na vikosi
vinavyounga mkono serikali wanaonekana kujipanga kutokana na uwezekano wa
shambulizi baada ya siku nyingi za mashambulizi ya anga dhidi ya waasi kusini
mwa Alepo.mashambulizi mapya yalianzishwa kwa msaada wa Urusi baada baada ya
kuvunjika makubaliano ya kusitisha vita kwa wiki nzima.
SHIRIKA LA AFYA LAHITAJI NJIA YA DHARURA ALEPO
Shirika la Afya Duniani limetoa wito wa mipango
ya haraka ya kuweka njia maalum ya kutokea Alepo kwa majeruhi na wagonjwa. Msemaji
wa shirika hilo amesema kwamba ni madaktari 35 tu waliobaki katika mji
unaoshikiliwa na waasi katika mji wa kusini kuwahudumia watu wanaokadiriwa kuwa
robo milioni.
No comments:
Post a Comment