LIGI YA KLABU BINGWA
BARANI ULAYA jana ilianza ambapo jumla ya michezo saba kwenye makundi matano ilipigwa kwenye viwanja tofauti.
Amabapo kundi
A Basel ya nchini uswiz
ilitoshana nguvu kwa kutoka suluhu ya moja kwa moja na Ludogorets Razgrad ya
nchini bulgaria, PSG ikiwa nyumbani ililazimiswa sare ya bao 1-1 dhidi ya
washika bunduki wa london Arsenal, huku PSG wakitangulia kupata goli la mapema
mnamo dk ya 1 ya mchezo kupitia mshambuliaji wake Edinson Cavani huku Goli la
kusawazisha kwa upande wa arsenal likivungwa na Alexis Sanchez kwenye dk ya 78.
Tukio kubwa katika mchezo huo ni kadi mbili nyekundu zilizotolewa kwa timu zote
mbili, Olivier Geroud akipewa kadi nyekundu kwenye dk ya 90 ya mchezo baada ya
kadi ya njano aliyopewa kwenye dk ya 88, huku kwa upande wa PSG Marco Verratti nae
pia akiambulia kadi nyekudu kwenye dk hiyo hiyo ya 90 baada ya kadi ya njano
aliyopewa kwenye dk ya 8.
Lakini matokeo makubwa waliyapata Barcelona baada
ya kubamiza Celtic kwa idadi ya magoli 7-0 huku messi akianza na hat- trick,
magoli mengine yalifungwa na Suarez ambaye alipachika magoli mawili, Neymar na
Iniesta wakipata goli moja moja. Huku Mousa Dembele akikosa mkwaju wa Penalt
kwa upande wa Celtic
Na mchezo mwengine wa kundi D Bayern Munich ilicharanga FC Rostov ya nchini
Urusi Magoli 5-0 huku Atletico Madrid ya nchini Uispania ikiwa ugenini iliibuka
na ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya mwenyeji wake PSV Eindhoven ya nchini
uholanzi
Mechi nyengine ni
Benfica1 - 1 Besiktas
Dynamo Kyiv1 - 2 SSC Napoli
No comments:
Post a Comment