Tuesday, 27 September 2016

KIMATAIFA

MAPIGANO ALEPO YAPAMBA MOTO



Ripoti kutoka Alepo inasema vikosi vya serikali ya Syria vimeendelea kuimarika katikati mji huo. Waasi na vikosi vinavyounga mkono serikali wanaonekana kujipanga kutokana na uwezekano wa shambulizi baada ya siku nyingi za mashambulizi ya anga dhidi ya waasi kusini mwa Alepo.mashambulizi mapya yalianzishwa kwa msaada wa Urusi baada baada ya kuvunjika makubaliano ya kusitisha vita kwa wiki nzima.

 

SHIRIKA LA AFYA LAHITAJI NJIA YA DHARURA ALEPO
Shirika la Afya Duniani limetoa wito wa mipango ya haraka ya kuweka njia maalum ya kutokea Alepo kwa majeruhi na wagonjwa. Msemaji wa shirika hilo amesema kwamba ni madaktari 35 tu waliobaki katika mji unaoshikiliwa na waasi katika mji wa kusini kuwahudumia watu wanaokadiriwa kuwa robo milioni.
 

No comments:

Post a Comment