Meneja wa
mashetani wekundu Jose Mourinho amesema michuano ya Europa inaweza kuathiri
timu yake malengo ya ubingwa wa ligi kuu ya England . lakini bado anataka
kushinda kwenye hatua ya pili ya michuano hiyo ya Europa na atahakikisha
wachezaji wake wanakuwa tayari kwa pambano.
Kikosi cha
Man.U kikiwa na wachezaji 20 bila nahodha wao wayne rooney kikiwa ugenini leo
hii kitakipiga na fayenoord ya uholanzi
Ligi ya klabu
bingwa barani ulaya imeedelea kutimua vumbi usiku wa kuamkia leo ambapo
kulikuwa na michezo tisa ikipigwa katika viwanja tofauti.
KATIKA USIKU WA KLABU BINGWA KUAMKIA LEO
Matajiri wa london Manchester City
wakiwa nyumbani waliibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Borussia
Moenchengladbach, hatrick ya Kun Aguero na goli moja la Kelechi Iheanacho yalitosha kuipatia man.city point
tatu na kuwa timu ya pili kwenye msimamo wa kundi C ambalo linaongozwa na
Barcelona
Tottenham Hotspurs
ikiwa nyumbani ilikubali kipigo cha magoli mawili kwa moja dhidi ya Monaco ya nchini
Ufaransa ambayo inaongoza ligi kuu nchini humo
Lakini usiku wa
kuamkia leo ilikuwa ni kicheko kwa wachezaji na washabiki wa Leicester City
Kwani wakiwa ugenini waliipiga Club Brugge ya
ubelgiji jumla ya magoli 3-0 huku Riyad Mahrez
akitupia mawili.
Borussia Dortmund
ikiwa ugenini iliidhalilisha Legia Warszawa ya Poland kwa dozi ya magoli 6-0
Na katika mchezo uliowastaajabisha wengi
ulikuwa ni mchezo kati ya Real Madri dhidi ya Sporting CP Lisbon ya ureno ambapo Madrid
iliibuka na ushindi wa magoli 2-1.
No comments:
Post a Comment