Timu ya taifa ya Sweden ya
wanawake imefuzu kuingia hatua ya makundi michuano ya EURO 2017 baada ya
kuifunga Slovakia, Ublgiji na Romania.
Andy Murray ambaye anashikilia
namba mbili kwa ubora duniai atacheza na aliyekuwa bingwa wa michuano ya wazi
ya Marekani Juan Martin del Potro ikiwa ni mchezo kwanza wa kombe la
Devis katika hatua ya nusu fainali utakao pigwa mjini Glasgow Scotland leo saa
13:00 mchana.
Del Potro ambaye yupo nafasi ya
64 kwa ubora duniani na amerejea kutoka majeruhi, alipotez pambano dhidi ya
Murry kwenye michuano ya olimpic mjini rio mwezi uliopita.
Lakini pia ndugu wawili Andy na
Jamie Murraywatacheza pamoja siku ya jumamosi katika mchezo wa pamoja
wakiiwakilisha timu ya Uingereza
Davis Cup linachukuliwa
kuwa ndilo kombe la dunia la tenis ambalo husimamiwa na shirikisho la tennis la
dunia ITF.
West Bromwich Albion inayoshiriki ligi kuu England
imetangza kuwa mpango wa kiuza klabu hiyo kwa waekezaji kutoka Uchina
umekamilika
Aliyekuwa mwenyekiti wa clabu hiyo Jeremy Peace
alikubali mpango wa kuiuza kwa kampuni ya ushirika inayoongozwa na mjasiriamali
Guochuan Lai kutoka Uchina
Mpango huo unahitimisha uenyekiti wa Jeremy Peace
ambaye ataondoka baaya ya kuimiliki timu hiyo kwa miaka 15. Nae mwenyekiti mpya
amemshukuru Jeremy Peace kwa kwa uongozi wake kwa kipindi cha miaka 15 na
kutengeneza misingi imara kwa hatua nyengine ya maendeleo ya klabu hiyo.
Michuano ya Uefa
ndogo au EUROPA imeanza katika hatua ya makundi, mechi zaid ya 20 zimechezwa
ambapo Manchester United ikiwa ugenini ilipokea kichapo cha kukera cha bao moja
kwa bila dhidi ya Feyenoord ya uholanzi.
Na klabu ya Genk ya ubelgigi anayochezea ndugu
yetu mbwana samata pia ikiwa ugenini imepokea kichapo cha magoli 3-2 dhidi ya Rapid
Wien ya Austria. Mbwana Samata alitolewa kwenye Dk
ya 78 na nafasi yake kuchukuliwa na Nikos Karelis.
Na ligi kuu
England hapo kesho Jumamosi kutakuwa na michezo mitano ambapo Hull City itamkaribisha Arsenal, mabingwa watetezi
Leicester City watamkaribisha Burnley, matajiri wa London Manchester city
wataialika AFC
Bournemouth, west Bromwich ambayo imepata mwenyekiti mpya itamualika west ham
na Everton wakiwa nyumbani watawaalika
Middlesbrough. Michezo yote itapigwa saa 17:00 ispokuwa mchezo wa mwisho kati ya everton na Middlesbrough ambao utachezwa saa 19:30
Middlesbrough. Michezo yote itapigwa saa 17:00 ispokuwa mchezo wa mwisho kati ya everton na Middlesbrough ambao utachezwa saa 19:30
Katika msimamo wa
michuano ya olimpic ya walemavu paralimpic hadi sasa Uchina inaongoza kwa idadi
ya medali ikiwa na jumla ya medali 191 ikifuatiwa na uingereza yenye jumla ya
medali 107 na nafasi ya tatu ni Ukrain yenye medali 92. kwa Afrika Nigeria inashikilia nafasi ya kwanza ikiwa na medali 12 ambayo ni ya 11 katika msimamimo wa jumla ikifuatiwa na Africa Kusini.
No comments:
Post a Comment