Tuesday, 27 September 2016

RAIS WA ZAMANI WA ISRAEL AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 93


Ripoti kutoka Israel zinasemaaliyekuwa Rais na waziri mkuu wa Israel Simon Perez amefariki usiku wa kuamkia leo. Perez alikuwa amelazwa hospitali akiugua kiharusi. 
Ndugu wa karibu wamenda hospitali ambako amekuwa huko tangu alipouguwa kiharusi wiki mbili zilizopita. Shimon Peres amelitumikia taifa la Israel kwa kipindi cha miongo miwili tofauti akiwa kama waziri mkuu na Rais wa taifa hilo. Alishinda tuzo ya

Amani kwa chama chake kwa sera zake za kisiasa na Palestina kwenye miaka ya 1990. Ni miongoni mwa kizazi cha mwisho cha wanasiasa wa Israel amabao wawahi kuwa Marais wakati wa kuzaliwa kwa taifa jipya mwaka 1948.
 

AFYA YA RAIS WA ZAMANI WA ISRAEL YAZIDI KUZOROTA





Ripoti kutoka Israel zinasema afya ya mwanasiasa na Rais mstaafu  Shimon Peres inaendelea kuzorota.Ndugu wa karibu wamenda hospitali ambako amekuwa huko tangu alipouguwa kiharusi wiki mbili zilizopita. Shimon Peres amelitumikia taifa la Israel kwa kipindi cha miongo miwili tofauti akiwa kama waziri mkuu na Rais wa taifa hilo. Alishinda tuzo ya Amani kwa chama chake kwa sera zake za kisiasa na Palestina kwenye miaka ya 1990. Ni miongoni mwa kizazi cha mwisho cha wanasiasa wa Israel amabao wawahi kuwa Marais wakati wa kuzaliwa kwa taifa jipya mwaka 1948.

TIMU ZA KAMPENI ZARIDHISHWA NA WAGOMBEA WAO



TIMU ZA KAMPENI ZA URAIS ZARIDHISWA NA MAJIBU YA WAGOMBEA


Timu za kampeni kwa Hillary Clinton na Donald Trump wote wameridhishwa na mwenendo ya wagombea wao katika mdahalo wao wa kwanza wa televisheni wa kampeni za urais Marekani. Wagombea hao mahasimu wa walikuwa wakikwazana mara kwa mara. Bwana Trump alimshtumu bi Clinton  kwa kuwa mwanachama wa uzalishaji mbovu wa kisiasa. Na Bi Clinton alisema mhasimu wake amekuwa ni aina ya mtu ambaye anawezakukasisishwa na twita na asingepaswa kunyoosha vidole vyake popote karibu na kodi za Nuclia za Marekani.
 


SHAMBULIO BAGHDAD LOAWAUWA WATU 11 NA KUJERUHI ZAID YA 50
Shambulio la bomu katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad,limewauwa watu kumi na mmoja na kuwajeruhi zaid ya watu hamsini. Kundi la I-S limedai kuhusika kwa mashambulio hayo,likisema mmoja ya wapiganaji wake alijilipua katika eneo linalokaliwa na waislimau wengi wa madhehebu ya shia mjini Baghdad wilaya ya Jadida,likiwauwa watu nane. Shambulio jengine lililenga la mauwaji lililenga eneo la Bayaa kusini mwa Baghdad,likiwauwa watu tisa.Mwaka huu umeshuhudiwa idadi kubwa ya mashambulizi ya I-S katika mji mkuu wa Iraq, wakati kundi hilo likipoteza baadhi ya majimbo maeneo mengine ya nchi hiyo.