Balozi wa marekani
katika umoja wa mataifa, Samantha Power ameituhumu urusi kwa
kuzungumza uongo uliodhahiri kuhusu hatua yake nchini syria. Amesema kuwa
warusi hawakushirikishwa katika kupamana na ugaidi nchi Syria. Bi Power
aliliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamaba urusi na Syria wanatekeleza
vitendo vyote vya kimabavu dhidi ya upinzani uliopo mashariki mwa Alepo, ndipo
hapo uhalifu wa kivita unaweza kutekelezwa kwa kirahisi. Kwa upande mwengine
Balozi wa Urusi, Vitaly Churkin, amewatuhumu waasi kwa kuvunja makubaliano ya
kusitisha vita amabyo yalishindikana ndani ya muda mchache tu. Na muwakilishi
wa Syria ameliambia baraza hilo la usalama kwamba jimbo lote la Alepo litarudishwa
mikononi mwa serikali.
Umiliki wa
jimbo la Alepo kwa waasi umeendelea kupungua ikiwa ni jitihada za urusi kuinga
mkono serikali ya Syria katika kutekeleza mashambulizi dhidi ya waasi. Watoa huduma
za matibabu wamesema kuwa wameshuhudia mashambuliza ya anga katika maeneo
jirani ya kusini mwa mji huo. Mdadisi wa haki za binadam wa Uingereza aliyepo
nchinim Syria amesema kuwa zaidi ya watu 20 wameuwawa, na kiasi hicho cha
mauwaji kinatarajiwa kuongezeka. Kuna baadhi ya wakazi wamezingirwa na kifusi
katika majengo yaliyoharibiwa, na watowa huduma za matibabu kwa mara nyengine
wamezidiwa.
Wapiga kura
wa uswizi wameidhinisha sheria ya kuipa nguvu ya ziada kitengo cha ujasusi cha
nchi hiyo. Matokeo ya mwisho ya kura yameonesha kuwa takriban asilimia 66 ya
kura wameunga mkono. Sheria hiyo itaruhusu mamlaka kuchunguza simu,kufuatilia
shuguli za mitandao na kutumia kamera za siri na vipaza sauti kumchunguza
mshtakiwa. Mwandisi wa BBC anasema kwamaba katika kipindi kilichopita Uswizi
ilikuwa na wasiwasi kuhusu kuongeza mamlaka ya ufatiliaji ya nchi. Lakini shambulio
la kigaidi la hivi karibuni lililotokea nchi jirani ya Ufaransa limebadilisha
fikra za watu wengi.
Wabosnia na
Waserbia wamepiga kura ya kuamua kwamba Januari tisa iwe ni siku ya mapumziko
au la licha ya kuwa kura hiyo imepigwa marufuku na mahaka ya juu nchini Bosnia.
Tarehe hiyo inahusiana na siku ya karamu kwa wakiristo wa madhehebu ya Othodox, na mahakama imesema kuwa huo ni ukandamizaji
dhidi ya waisilamu wa Bosnia na wakiristo wa mahdhehebu ya katoliki wa Krosia
wanaoishi nchini Serbia. Januari tisa pia ilikuwa ni tarehe mwaka 1992 amabayo
Serbia iliwatangazia uhuru wa Croshia ndani ya Bosnia, iliyopelekea mtafaruku
wa kimaadili. Mwandishi wa BBC nchini
Serbia anasema kuwa sheria hiyo imeandaliwa ili kuchochea uchaguzi wiki ijayo.
Rais Francois
Hollande amekiri kuwa ufaransa iliwatelekeza walgeria walipigana vita wakiwa
upande wa Ufaransa wakati wa Vita ya uhuru ya Ageria iliyodumu miaka nane
iliyomalizika mwaka 1962. Makumi kati ya maelfu ya wa Algeria waliojitolea
kwenye vita wajulikanao kama ‘hakins ’ waliwawa kama wasaliti baada ya Ufaransa kuondoka Algeria. Wale wote
waliofanya hivyo kwa ajili ya Ufaransa walihifadhiwa kwenye kamabi. Katika sherehe
mjini Paris ikiashiria siku ya kitaifa ya kuwaheshimu waliojitolea kwa vita,
rais Hollande alisema ufaransa inabeba lawama kwa jinsi walivyofanyiwa. Vizazi vyao
walitafuta kwa muda mrefu utambuzi rasmi wa dhuluma.
waziri wa
mambo ya nje wa somalia, Abdisalam Hadliyeh anasema kwamamba kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al Shabaab
limeshindwa kijeshi, kwa ushirikiano wa jeshi la Somalia na vikosi vya kulinda Amani
vya umoja wa Afrika. Waziri huyo amesema
kwamba Al Shabaab kwa sasa wanamiliki chini ya asilimia kumi ya nchi nzima , na
viongozi wake wengi wameuwawa au kukimbia katika miezi ya hivi karibuni. Hadliyeh
amesema kuwa jambo lililopelekea utulivu wa muda mrefu ni kuwa na vifaa vizuri,
mafunzo ya kijeshi na kufadhiliwa vikosi vya usalama vya taifa. Mchambuzi wa
BBC wa masuala ya Afrika anasema kwamba licha ya kuwa kundi hilo limetokomezwa
kwenye mji mkuu wa Mogadishu, lakini
bado linaendesha mashambulizi ya mara kwa mara mjini hapa na kwengineko.
Polisi nchini
hungary wanasema mlipuko wa Budapest usiku wa jumamosi uliowajeruhi maafsa
wawili wa polisi ulisababishwa na bomu la kienyeji. Mkuu wa jeshi la polisi wa
hungary Karoly Papp amesema afsa wa
palisi aliyekuwa kwenye patro akitembea kwa miguu alilengwa na shambulio hilo. Kwasasa
wapo katika hali nzuri wakiwa Hospitali. Mtu anaeshtumiwa kutekeleza shambulio
hilo, anaelezewa kuwa ni kijana wa miaka
ishirini bado hajapatikana.
Tamasha
nchini Urusi la mpiga picha anyetatanisha wa marekani limefungwa baada kupingwa na wanaharakati. Picha
ziliyopigwa na Jock Sturges inajumuisha picha
zinazomwonyesha mtoto akiwa mtupu. Seneta wa kihafidhina mwenye ushawishi
mkubwa na mshauri wa serikali kwa masuala ya watoto wote wamelielezea tamasha
hilo kuwa ni tamsha la ngono ya watoto na wametaka kufungwa kwa tamasha hilo. Mashuhuda
wanasema takriban wnaharakati ishirini
waliojiita kuwa ni maafsa wa Urusi walilifunga tamasha hilo mjini Moscow
na mmoja kati yao alirembea chupa ya mkojo juu ya baadhi ya picha hizo. Msimamizi
wa tamasha hilo alisema alikuwa analifunga tamasha hilo baada ya kuapat vitisho
kwa watu wadanganyifu.
Mmoja wa vijana
mashuhuri wa mchezo wa mpira wa kikapu, José
Fernandez, amefariki katika ajali ya boti katika fukwe ya Miami. Walinzi wa fukwe wa marekani wamethibitisha
kuwa Fernandez ni mmoja kati ya watu watatu waliokutwa wamekufa katika majira
ya mapema siku ya jumamosi baada ya doria.Klabu yake ya Miami Marlins, ilisema
imeghairisha mchezo wake wa siku ya jumapili ikiwa kama ishara ya
kumuenzi. Kijana wa miaka 24 Fernandez ni
mzaliwa wa Cuba. Alijaribu kuikosoa
serikali ya Cuba zaidi ya mara tatu, na akajikuta akiishia gerezani. Katika kipindi
chake cha mwisho alipofanikiwa kuingia Marekani mwaka 2007, mama yake alianguka
baharini Akajitosa na kufanikiwa kumuokoa.
Mwanamme mmoja
raia wa ureno ameweza kutembea kwa mara nyengine tena baada ya kutumia miaka 43
akiwa kwenye kiti cha kutembelea kutokana na utambuzi potofu wa Dawa. Mwanamme huyo
Rufino
Borrego, alikiambia chombo cha habari cha ureno kwamba mtaalamu wa mishipa ya
hisia (neurologist) ametambua baadada ya zaidi ya miaka 40 kwamba alikuwa
akisumbuliwa na maradhi tofauti kama vile myasthenia ambayo ni tofauti na
utambuzi wa awali wa muscular dystrophy ambayo inatibika. Wakati Borrego
alipoweza kutembea kwa mara ya kwanza kwenda kwenye mgahawa wa jirani
anaokwenda kila siku uliopo Alandroal, kusinimashariki mwa ureno, mmiliki wa
mgahawa huo alisema lidhani kuwa anaona muujiza mbele yake.
Beki wa Man
U Chris Smalling amesema Nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney hakuathirika kwa
lolote wakati alipotupwa benchi na bado ni mchezaji bora wa Old Traford,
Rooney
mwenye umri wa miaka 30 aliachwa nje ya
kikosi cha cha kwanza cha Jose Mourinho kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya mabingwa
watetezi Leicester katika mchezo ulipigwa siku ya Jumamosi
Mlinzi huyo wa
kati raia wa England ameongeza kuwa Rooney alikuwa ni yuleyule kabla ya mchezo
wakati tukijiandaa na mchezo.Yeye mara nyingi amekuwa ni mjadala na alikuwa
niyuleyule tuliyemzoea.
No comments:
Post a Comment