Maelfu ya watu wamehudhuria swala ya
kiislamu ya kumuombea aliyekuwa mwandondi bingwa duniani Muhammad Ali
-- ambae alikufa wiki iliyopita.
Swala hiyo imefanyika katika
ukumbi wa 'Freedom Hall' katika mji aliokulia wa Louisville.Waombolezaji
walisikika wakimpa sifa Muhammad Ali kwa kuulita jina lake wakati mwili
wa bondia huyo ulipoingizwa ukumbini.Viongozi wakubwa katika ulimwengu wa ndondi na wanaharakati walikuwa sehemu ya waliohudhuria.Swala imeongozwa na Imam wa California, sheikh Zaid Shakir, ambae alikuwa pembezoni mwa Muhammad Ali pindi alipokuwa anakata roho na kupata fursa ya kumwombea dua ya mwisho kabla ya maziko.
No comments:
Post a Comment