Pages

Thursday, 15 September 2016

MICHEZO MIX


Timu ya taifa ya Sweden ya wanawake imefuzu kuingia hatua ya makundi michuano ya EURO 2017 baada ya kuifunga Slovakia, Ublgiji na Romania.

Andy Murray ambaye anashikilia namba mbili kwa ubora duniai atacheza na aliyekuwa bingwa wa michuano ya wazi ya Marekani Juan Martin del Potro ikiwa ni mchezo kwanza wa kombe la Devis katika hatua ya nusu fainali utakao pigwa mjini Glasgow Scotland leo saa 13:00 mchana.

Del Potro ambaye yupo nafasi ya 64 kwa ubora duniani na amerejea kutoka majeruhi, alipotez pambano dhidi ya Murry kwenye michuano ya olimpic mjini rio mwezi uliopita.
Lakini pia ndugu wawili Andy na Jamie Murraywatacheza pamoja siku ya jumamosi katika mchezo wa pamoja wakiiwakilisha timu ya Uingereza
Davis Cup linachukuliwa kuwa ndilo kombe la dunia la tenis ambalo husimamiwa na shirikisho la tennis la dunia ITF.

West Bromwich Albion inayoshiriki ligi kuu England imetangza kuwa mpango wa kiuza klabu hiyo kwa waekezaji kutoka Uchina umekamilika
Aliyekuwa mwenyekiti wa clabu hiyo Jeremy Peace alikubali mpango wa kuiuza kwa kampuni ya ushirika inayoongozwa na mjasiriamali Guochuan Lai kutoka Uchina
Mpango huo unahitimisha uenyekiti wa Jeremy Peace ambaye ataondoka baaya ya kuimiliki timu hiyo kwa miaka 15. Nae mwenyekiti mpya amemshukuru Jeremy Peace kwa kwa uongozi wake kwa kipindi cha miaka 15 na kutengeneza misingi imara kwa hatua nyengine ya maendeleo ya klabu hiyo.

Michuano ya Uefa ndogo au EUROPA imeanza katika hatua ya makundi, mechi zaid ya 20 zimechezwa ambapo Manchester United ikiwa ugenini ilipokea kichapo cha kukera cha bao moja kwa bila dhidi ya Feyenoord ya uholanzi.

Na klabu ya Genk ya ubelgigi anayochezea ndugu yetu mbwana samata pia ikiwa ugenini imepokea kichapo cha magoli 3-2 dhidi ya Rapid Wien ya Austria. Mbwana Samata alitolewa kwenye Dk ya 78 na nafasi yake kuchukuliwa na  Nikos Karelis.

Na ligi kuu England hapo kesho Jumamosi kutakuwa na michezo mitano ambapo Hull City itamkaribisha Arsenal, mabingwa watetezi Leicester City watamkaribisha Burnley, matajiri wa London Manchester city wataialika AFC Bournemouth, west Bromwich ambayo imepata mwenyekiti mpya itamualika west ham na Everton wakiwa nyumbani watawaalika
Middlesbrough.
Michezo yote itapigwa saa 17:00 ispokuwa mchezo wa mwisho kati ya everton na Middlesbrough ambao utachezwa saa 19:30


Katika msimamo wa michuano ya olimpic ya walemavu paralimpic hadi sasa Uchina inaongoza kwa idadi ya medali ikiwa na jumla ya medali 191 ikifuatiwa na uingereza yenye jumla ya medali 107 na nafasi ya tatu ni Ukrain yenye medali 92. kwa Afrika Nigeria inashikilia nafasi ya kwanza ikiwa na medali 12 ambayo ni ya 11 katika msimamimo wa jumla  ikifuatiwa na Africa Kusini.

No comments:

Post a Comment